Na Elinipa Lupembe
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mkoa wa Arusha, wamemkabidhi Tuzo ya Uongozi Uliotukuka, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, mara baada ya kuridhishwa na uongozi wake, unaokwenda sambamba na usimamizi wake thabiti wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo mkoani Arusha.
Wajumbe hao, wakiongozwa na Mwenyekiti ALAT Mkoa wa Arusha, na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian Matle Iranghe, wameuelezea uongozi wa Mhe. Mongella, kuwa ni uongozi uliotokuka ndani ya mkoa, uliwaunganisha watu wa Arusha licha ya mgawanyiko wa kisiasa, uliokuwepo kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza mkoa huo wa Arusha wenye pilika nyingi za kimaisha.
Mhe. Maximilian, amesema kuwa, wajumbe wa ALAT mkoa, wameamua kumpa tuzo hiyo, si kwa ushabiki bali ni kutokana na kuridhishwa na hali ya utulivu wa wananchi wa Arusha, uliwawezesha kuachana na malumbano ya kisisasa, na kujikita zaidi kwenye shughuli za uzalishaji mali kwa maelendelo ya mtu mmoja mmoja, mkoa na Taifa.
"Arusha ni mkoa wa kimkakati, ukisheheni wakazi wenye heka heka nyingi, uwepo wa uongozi imara wa Mhe. Mongella umeondoa mpasuko uliokiwepo uliotokana na itikadi za kisiasa, na kuthibitisha kuwa Mhe. Mongelle ameweza kuwaunganisha wanaArusha na kuwa kitu kimoja sasa, tunampongeza sana, tunampa maua yake"Amesema
Aidha, amemuelezea Mhe. Mongella ni kiongozi muwazi, asiye na mbili, mara nyingi amekuwa akisema ukweli kwa kupambana, na kuhakikisha amani na utuivu, huku miradi yote inatekelezwa kwa kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, amempongeza, Mhe. Mongella kwa kazi nzuri anayoifanya, na kuhakikisha usalama wa mkoa, unasababisha wananchi wake kujikita kwenye kufanya shughuli za maendeleo na si malumbano.
Ameweka wazi kuwa, Mhe Mongella amekuwa msimamizi mzuri wa miradi yote ya maendeleo, inayofanyika kwenye halmashauri zake, bila kubagua, akiweka mbele maslahi ya Umma, ambayo wamekiri na kushuhudia ikitekelezwa na kukamilika kwa wakati, huku ikizingatia viwango vya ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.
Hata hivyo Mhe. Mongella amewashukuru Wajumbe hao wa ALAT kwa kuona anastahili kupewa tuzo hiyo, huku akiwataka kuendeleza umoja na mshikamamo miongoni mwao, ili wananchi waige kutoka kwao, kwa kuwa wao ni viongozi wawakilishi wa wananchi.
Amesema kuwa, wananchi wa mkoa wa Arusha, wanatambua na kuthamini umuhimu wa amani na utulivu, ulipo sasa huku wakiejitoa kufanya kazi za kujitafutia kipato jambo ambalo linamuunga mkono kwa vitendo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, anaye wahimiza waTanzania kufanya kazi, huku ikithibitishwa na agenda yake ya Kazi Iendee kama kipaumbele chake.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.