Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella ameshiriki hafla fupi ya kumuaga, Kamishina Mstaafu wa Uhifadhi - TANAPA, Dkt. Allan Herbert Kijazi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Aim Mall, Jijini Arusha, hafla iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi ya Tanzania - TANAPA
Mhe. Mongella amempongeza kiongozi huyo makini, aliyelitumikia Taifa la Tanzania kwa nyadhifa mbalimbali alizokuwa nazo kwa uaminifu na hatimaye kustaafu kwa heshima, kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma.
Amesema kuwa Katika Utumishi wa Dkt.Kijazi serikali imenufaika kwa kupata mafanikio makubwa kupitia utumishi wake, na kuongeza kuwa mkoa wa Arusha unajivunia mchango mkubwa wa TANAPA, katika kukuza pato la mkoa na kwa mtu mmoja mmoja, kipindi chote alichoitumikia TANAPA.
"Nichukue fursa hii adhimu kukupongeza kwa mafanikio yako makubwa katika utumishi wa umma na sisi kama mkoa wa Arusha tunatambua mchango wako kupitia TANAPA ambao ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na hasa katika mkoa wetu kwa kuwa makao makuu yake yapo hapa."
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.