Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella ameshiriki Misa takatifu ya kumuaga Askofu Mstaafu, Paulo Ruzoka na kumtakia utume mwema mwandamizi wake, Mhasham Askofu Protase Kadinali Rugambwa wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, aliyechukua nafasi hiyo.
Akitoa salamu za Serikali kwenye Misa hiyo takatifu, kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dotto Biteko, Serikali itaendelea kupokea maoni ya viongozi wa dini na watanzania wengine ili kuliwezesha Taifa kusonga mbele kwenye nyanja zote za maendeleo.
Amesema kuwa Mhe. Rais anaendelea kumpa shirikiano baba Askofu Rugambwa na
na yuko pamoja naye, huku akitegemea mengi kutoka kwake, ikiwemo maoni na ushauri kwa serikali, pamoja na kuwaelekeza wanaTabora kumtii Mungu na Serikali yao, jambo ambalo litaendeleza amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
"Tunaweza kutofautiana kwenye mitazamo na maoni, tunaweza kutoautina kwenye misimamo wa kidini lakini kamwe tusivunje umoja wa kitaifa, tupambane kuwaondoa watanzania kwenyw umasikini na kuwaletea nafuu kubwa ya maisha, wanaohitaji maji, barabara na umeme, tuwapeleke" Amesema Naibu Waziri.
Hata hivyo Maaskofu hao kwa pamoja Askofu Mstaafu Kazoka na Mhasham Askofu Kardinali Rugambwa, wamemshukuru Rais Samia kwa ujumbe na ahadi yake ya ushirikiano na kanisa, na kuthibitisha kuwa yapo mengi hushirikiana naye na serikali kwa ujumla wake, kanisa litayaendeleza vema
Katika Misa hiyo, Mkuu wa mkoa Arusha, ameungana na mwenyeji wake, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Dkt. Batilda Burihan kushiri katika misa hiyo maalumu leo 19.11.2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.