Na Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amezindua kadi ya kielektroniki ya Kimataifa ya huduma za kifedha 'Amercan Express CARD',itakayotumika kwenye Mashine za ATM, programu inayoendeshwa kwa ushirikiano wa benki ya CRDB - Tanzania, hafla iliyofanyika kwenye hotel ya Gran Melia, mkoani Arusha.
Mhe. Mongella licha ya kuupongeza uongozi wa benki ya CRDB kwa mkakati huo muhimu kwa watanzania na wageni wakimataifa, amewashukuru kwa kuchagua mkoa wa Arusha, kuwa ndio eneo stahili la kufanya uzindua wa programu hiyo ya kimataifa.
Ameweka wazi kuwa, Benki ya CRDB ni benki inayojulikana ndani na nje ya nchi, na kupitia Kauli Mbiu yake ya "Ulipo Tupo", ambayo imewafanya watumia huduma rasmi za fedha kuifahamu zaidi benki hiyo, inayosaidia kuimarika na kukua kwa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa, Huduma ya Express Card itasaidia kurahisisha upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha, hasa kwa kuzingatia asilimia 80 ya shughuli na biashara za utalii nchini, zinafanyika mkoani Arusha, wadau wa utalii wanatambua nafasi ya utalii, licha ya kuwasaidia wenyeji zaidi itawasaidia wageni wanaofika na kupita Arusha kila iitwayo leo" Amesema Mhe. Mongella.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, kwa niaba ya Bodi ya Benki ya CRDB na Menejimenti, Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Neema Mongi, amesema dhamira ya CRDB ni kuboresha na kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma rasmi za kifeha ndani na nje ya nchi, huku kipao mbele, kikiwa ni kutambua umuhimu wa huduma bora na za kisasa pamoja na kukidhi mahitaji ya wateja.
"CRDB Bank, imendelea kutafuta njia tofauti za kukidhi mahitaji ya wateja wetu, kwa kubuni mifumo tofauti ya malipo kupitia kadi za kielekroniki, zaidi CRDB imefanikiwa kuungamisha biashara zaidi ya 3900, kwa kuanzisha huduma ya Tembo Kadi na TANAPA kwenye utalii wa ndani" Amesema Prof. Neema
Awali, Makamu wa Rais, Amercan Express Card, EMEA, Briana Wilsey, ameipongeza Benki ya CRDB kwa juhudi na mipango thabiti ya kuhakikisha hudama za kifedha zinawafikia wateja kwa wakati kupitia mifumo ya kielekroniki ambayo inatumika duniani kote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.