Mwenyekiti wa kamati ya riadha Mkoa wa Arusha bwana Richard Kwitega,amesema mchezo wa riadha ni nembo kubwa kwa mkoa wa Arusha.
Ameseyasema hayo alipokuwa akiwapokea wanaridha mbalimbali walioshiriki katika maandalizi ya kuwapata wanariadha wa Mkoa kutoka taasisi mbalimbali za serikali na binafsi na vyama vya riadha vya mkoa wa Arusha.
Amewataka viongozi wa chama cha riadha Mkoa wa Arusha kuhakikisha mbio hizo zinaendelea kufanyika kila mwaka ili kuwaandaa washiriki wazuri katika ngazi ya Mkoa.
Nae, katibu tawala msaidizi upande wa elimu bwana Halfani Omari Msukila amesema michezo ni tasnia yenye umuhimu mkubwa sana kwani inatengeneza ajira na kujenga afya.
Pia, amewataka wafanyabiashara mbalimbali kutumia fursa za michezo kutangaza biashara zao, kwani ni njia moja wapo ya kukuza uchumi wao.
Amesema serikali itaendelea kushirikiana na vyama mbalimbali vya michezo vya mkoa wa Arusha ili kuhakikisha michezo inakuwa kwa haraka zaidi.
Mbio hizo zilijumuisha zaidi ya wanariadha 200 kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali kwa Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.