Tunapenda kuongeza nguvu kwa wakala wa barabara vijijini (TARURA) waweze kujenga barabara nyingi vijijini na kuongeza nguvu kwa wakala wa usambazaji maji vijijini Ruwasa iliwaweze kutoa huduma ya maji vijijini. Kama tuvyosema kwenye ilani na ahadi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hasssan wakati akisalimiana na wananchi walijitokeza kumpokea TFA wilayani Karatu Mkoa wa Arusha. Amesema wingi wa watu ulimpokea Karatu unaonesha namna gani wananchi wanatamani viongozi waje kuwatembelea.
Amesema kuanzia mwezi wa kumi na moja ataanza ziara upande wa kaskazini mwa Tanzania, amesema kwa sasa anafanya ziara maalumu ya kuchukua filamu kwa ajili ya kutangaza vivutio kwenye utalii kwa lengo la kuhamasisha uwekeza na wageni waje kututembelea.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.