Angela Msimbira ARUSHA
Wananchi wa Kata ya Mwandet Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwajengea Kituo cha Afya cha Mwandet ambacho kimesaidia kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Engutoto Jafet Simon ameyasema hayo kwenye ziara ya mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt.Rashid Mfaume alipotembelea kituo cha Afya cha Mwandet kilichojengwa katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua miundombinu pamoja na hali ya utoaji wa huduma za afya.
Amesema kituo hicho kitasaidia wananchi takribani 23,995 kutoka vijiji vya Imbibia,Eunoto,Engalaoni, Engutoto na kijiji cha Mferejini kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ambao walikuwa wakifuata huduma katika Hospitali ya Mount Meru.
Naye, Joseph Sanare amepongeza Serikali kwa kuendelea kuwajali wananchi kwa kuwasogezea huduma muhimu za afya kwenye maeneo yao.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mwandet Aidan Martin amesema jumla ya sh. milioni 740 kutoka Serikali kuu, tozo na UVIKO-19 kwa ajili ya jengo la mama na mtot, jengo la wagonjwa wa nje,maabara, jengo la X-ray,chumba cha kufulia na nyumba za watumishi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.