Serikali ya awamu ya sita, katika kutekeleza mkakati wa kuboresha na kuimarisha, hali ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, imetoa magari mengine matano kwa ajili ya wagonjwa wa dharura katika mkoa wa Arusha.
Akikabidhi magari hayo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amesema kuwa, mkoa huo, ni miongoni mwa mikoa iliyonufaika sana na ongezeko la bajeti ya Serikali katika sekta ya afya, kwa kupata fedha nyingi zilizotekeleza miradi ya ujenzi wa miundo mbinu pamoja na dawa, vifaa na vifaa tiba.
Mpaka kufikia mwezi Januari 2024, tayari mkoa huo umepokea jumla ya magari mapya 14 kwa awamu tatu mfululuzo, magari ya usimamizi shughuli za afya, magari ya huduma za wagonjwa wa dharura (ambulance) na lori la kutolea huduma tembezi 'mobile clinic'.
Mhe. Mongella, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali ya awamu ya sita, kwa kutoa vitendea kazi katika sekta ya afya, licha ya kurahisisha kazi, vinavyokwenda kuboresha hali ya utoaji na upatikanaji rahisi wa huduma za afya kwa wananchi hususani wagpnjwa dharura kupitia magari hayo
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.