Sheikh wa mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma kwaniaba ya Viongozi wa dini Mkoani Arusha ameongoza sala maalum kwaajili ya Kumuombea Kheri Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kutokana na kasi yao katika kuwaletea maendeleo wakazi wa mkoa wa Arusha.
Sheikh wa Juma ameongoza sala hiyo maalum leo Jumapili Novemba 17, 2024 kwenye Hafla ya kutoa tathimini ya utendaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita, akisema yaliyotendeka kwa kipindi hicho cha miezi sita ni maendeleo ambayo hayawezi kuhesabika kwa haraka.
Sheikh Juma ameungana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pia kusisitiza umuhimu wa amani nchini Tanzania, akisema suala hilo la amani ndilo linalochagiza maendeleo ya haraka kwenye mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.