Joseph K. Edward - Ngorongoro
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangwala, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa shule mpya ya sekondari Masusu katika kata ya Pinyinyi na kuridhidhwa na hatua za utekeleaji wa mradi huo na kuwapongeza mafundi na wananchi wa Pinyinyi kwa kujitoa kutekeleza mradi huo huku akiagiza kukamilika kwa jengo la utawala ndani ya siku tatu.
Aidha ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za kutekeleza na ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo huku mradi wa shule ya Masusu sekondari ukiwa ni nuru kwa watoto wa Panyinyi.
"Mhe. Rais ameendelea kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo kisekta mirafi ambayo inalenga kutatua changamoto nyingi za wananchi wa Ngorongoro, ni jukumu letu kusimamia miradi na kuhakikisha miradi yote inaleta matokeo yaliyokusudiwa na serikali" Amesema Mhe. Mangwala
Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Masusu, Mhe. Daniel Taiko Mollel ameishukuru serikali ya awamu ya sita, kwa ujezni wa shule mpya ndani ya kitongoji chake, shule ambayo licha ya watoto kusoma karibu na nyumbani itaondoa changamoto ya watoto kuacha shule kutokana na ndoa za utotoni.
"Sisi wananchi wa Masusu, tunajisikia furaha kwa kujengewa shule ya sekondari, hatukuwahi kuwa na shule kijijini kwetu, tunajivunia kuwa na Rais mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru sana kwa kutukumbuka" Amebainisha
Kiongozi wa mila, Laigwan Joshua Mang'atinda hakusita kutoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kujenga shule ya sekondari Masusu na kumshukuru mkuu wa Wilaya na watalamu wake kwa usimamizi wa karibu na kuhakikisha mradi unakamilika kwa kuzingatia vigezo vya ubora.
" Watoto wetu walilazimika kutembea umbali wa Km 10 mpaka 15 kufuata shule kata za jirani, mradi huu ni mkombozi wa watoto wetu, tuko tayari kufanya kazi usiku na mchana ili shule hii ikamilike haraka na watoto wetu waanze kusoma mapema Januari 2024" alihitimisha Lagwanan.
Sevelin Erasto mwalimu wa Sale sekondari na msimamizi wa mradi amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa fedha za Serikali kupitia mradi wa Kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari Nchini (SEQUIP)
Ikumbukwe kuwa miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020.
"CCM inaamini kuwa elimu bora ndiyo nyenzo muhimu ya kujenga, kulea, na kuendeleza rasilimaliwatu ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa Taifa na maendeleo ya jamii kwa ujumla". bara ya 77.
#mamayukokazini
#kaziinaendelea.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.