Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, ameongeza siku ya kesho Jumatatu Julai 01,2024 ili kuwapa nafasi wagonjwa walioshindwa kukamilishiwa matibabu yao kwa siku saba za Kambi ya matibabu bure Arusha, yanayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh amri Abeid Jijini Arusha.
Amesema hayo alipotembelea na kuangalia maendeleo ya utoaji na upatikana wa huduma kwa wagonjwa wanaoendlea kumiminika kwenye kambi hiyo ya matibabu bure, ikiwa ni siku ya saba ya Kliniki ya Madaktari Bingwa na Mabingwa Wabobezi, iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha na wadau wengine wa Afya kwa siku saba, kuanzi tarehe 24 mpaka tarehe 30 Juni, 2024 ambapo leo ni siku ya saba na ya mwisho.
Mhe. Makonda amesema kuwa, wamekubaliana na madaktari na timu nzima ya madaktari bingwa, kuitumia siku ya kesho kutoa huduma kwa wagonjwa ambao tayari wamesajiliwa na matibabu yao bado hayajakamilika hivyo kulazimika kuongeza siku ya kesho ya Jumatatu kuwahudumia wagonjwa hao.
"Tumekubaliana na Daktari wetu wa mkoa pamoja na timu nzima ya madaktari bingwa walioko hapa, kuonheza siku ya kesho Jumatatu, hatutaongeza mtu mpya bali tumeiongeza siku hiyo maalum kwa watu wote waliofika hapa wapate huduma iliyowaleta kwenye viwanja hivi na huduma hizo bado hazijakamilika". Amesema Mhe. Makonda
Amesisitiza kuwa, itakuwa haina maana mwananchi amekuja tangu Alhamisi, mwingine analala kwenye uwanja huu (Sheikh Amri Abeid) na matibabu sio zoezi la dakika moja kwamba umeingia pale na kutoka umetibiwa, yapo matibabu yana process hivyo tumeionheza siku ya kesho ili wagonjwa waweze kukamilisha matibabu yao.
"Kuna mwingine tumemtuma ameenda kutoa sampuli, na baadhi yake zimetumwa mpaka Dar Es salaam kupata majibu, ukimwambia mtu huyo leo zoezi limeisha arudi nyumbami wakati safari yake ya matibabu haijakamilika utakuwa haujamtendea haki, lengo letu kila aliyeingia kwneye uwanja huu apate matibabu yake sahihi". Amesema
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.