Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Angellah Kairuki amewataka wataalamu kutoka ngazi za Mikoa na Halmashauri kwenda kusimamia miradi ya kuboresha na kuimarisha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa kufuata Miongozo, Sheria na Kanuni zilizowekwa.
Ameyasema hayo, alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu mbalimbali kutoka ngazi za Mikoa na Halmshauri kwa kanda ya Kaskazini, yaliyofanyika Jijini Arusha.
Mradi wa BOOST umelenga kujenga madarasa 12,000 kwa nchi nzima na shule salama takribani 1000 ,huku ukilenga kuongeza uwandikishaji wa wanafunzi shule za awali.
Pia, amewataka wakahakikishe afua zote za mradi zinatekeleza kwa wakati ikiwemo miundombinu ya shule.
Aidha, amesisitiza katika utunzaji wa nyaraka za miradi yote na kuwataka wataalamu hao kuiandika vizuri ili kutunza kumbumbuku.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ramadhani Kairima amesema kwa kanda ya Kaskazini jumla ya wanafunzi wakufunzi 274 watajengewa uwezo wa mradi huo.
Kairima amezitaka halmashauri zote kuufanya mradi huo kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao.
Mradi BOOST umezinduliwa rasmi Mkoani Arusha ikiwa ni Kanda ya Kaskazini iliyojumuisha Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Singida na Arusha .
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.