Rais Samia Samia Hassan Suluhu amesema kuwa yeye si mtu wa maneno mengi bali ni mtu wa vitendo zaidi na hata Watu wakisema yeye anasonga mbele katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha inawajengea uwezo vijana wa kesho katika sekta ya kilimo ,mifugo,biashara.
Alisema bado serikali inafungua njia kwaaajili ya sekta binafsi na inajipanga vema kuhakikisha vijana wanapata ajira ili kujikwamua kiuchumi
Alisema anataka kuona vijana wanajia uchumi imara kwa ustawi wa maisha yao na familia zao na kusisita kuwa kwa vijana wa vyuo serikali itaendelea kuhakikisha vijana wa vyuo vya kati ikiwemo kuhakikisha mifugo ni mali na kuinua uchumi.
Pia alisisitiza kuwa serikali inatafuta njia kwakaushirikiana na sekta binafsi kwaajili ya kutengeneza ajira ikiwemo kukusaya fedha kwaajili ya kuwatumikia wananchi
Kwa vijana wa bodaboda na machinga alisisitiza kuwa bado kunakazi kubwa ya kufanya na serikali itaendelea kutafuta fedha kwaajili ya kuwakwamua vijana
"Mimi sina maneno mengi ni vitendo tu wakisema mimi nasonga mbele, na tutaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta uwekezaji wenye tija zaidi"
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa soko la kisasa la Tengeru,Rais Samia alisema serikali natafuta fedha zaidi kwaajili ya ujenzi wa soko la kisasa la Tengeru.
Awali,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongella alimshukuru Rais Dk,Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Alisema Mkoa wa Arusha umepata madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.