TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI
MAKABIDHIANO YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, inapenda kuutaarifu Umma kuwa, hafla fupi ya Makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha inatarajiwa kufanyika siku ya kesho, Jumatatu tarehe 08 Aprili 2024, kuanzia saa 03:00 asubuhi, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Katika hafla hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John V.K Mongella atamkabidhi Ofisi kwa mujibu wa taratibu Mkuu wa Mkoa mpya, Mhe. Paul Christian Makonda.
Aidha, baada ya shughuli za Makabidhiano ya kiofisi kukamilika, Mhe. Makonda atawasalimia wananchi watakaokuwa wamejitokeza kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hivyo wananchi wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi, kwa ajili ya kumpokea pamoja na kushiriki katika tukio hilo muhimu la kihistoria ambalo linadumisha umoja na mshikamano baina ya wananchi na Uongozi wa Mkoa wetu.
Awali, wageni waalikwa na wananchi wote wanasisitizwa kufika mapema kuanzia saa 01: 30 asubuhi na kuhudhuria kwenu ni muhimu kwa maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
OFISI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.