Katibu mkuu wa wizara ya habari,Utamaduni,sanaa na michezo, Suzan Mlawi amesema,Taifa lisilo na utamaduni ni taifa linalokufa na kutoa kizazi kisichoweza kuenzi na kuthamini mila na desturi zao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua tamasha la Urithi wa Utamaduni katika mkoa wa Arusha lililoanza Octoba 8, 2018 hadi Octoba 13 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
“Nimefarijika kuona tamasha hili litakuwa linafanyika kila mwaka, kwani litatoa nafasi kubwa sana kwa watanzania kujifunza tamaduni mbalimbali na pia litaenzi mila na desturi zetu kwa kiasi kikubwa”,alisema.
Amesema kupitia tamasha hili anategemea kuona ukuaji wa uchumi kwani bidhaa nyingi za asili zitapata masoko,kufufua mila na desturi zilizokufa kwa vijana wa sasa.
Mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi Pro.Audax Mabula, amesema tamasha hili lilizinduliwa mnamo Septemba 15,2018 na makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu Hasan mjini Dodoma na kuendelea Zanzibar, Dar es Salaam na sasa lipo mkoani Arusha.
Amesema lengo kubwa la tamasha hili ni kuenzi mila na malikale za Kitanzania kwani ni kwa mda mrefu sasa utamaduni wa watalii ndio umekuwa ukipewa kipaombele zaidi kuliko huu utalii wa utamaduni.
Kupitia tamasha hili la urithi wa utamaduni itasaidia kuutambulisha zaidi urithi wa utamaduni katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Nae katibu tawala wa mkoa wa Richard Kwitega amesema tamasha hili kwa mkoa wa Arusha litasaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mila na desturi za makabila ya mkoa huu na pia kuwakutanisha makabila mbalimbali na kuweza kujifunza tamaduni zetu.
Tamasha hili la urithi wa utamaduni lilizinduliwa kwa mala ya kwanza nchini jijini Dodoma na litakuwa likifanyika kila mwaka kwa mwezi mzima wa Septemba katika mikoa mbalimbali na kwa Mkoa wa Arusha linafanyika pia katika wilaya ya Karatu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.