WAFUGAJI nchini wataanza kupatiwa mbegu bora zangombe wa kisasa kwa gharama nafuu baada ya Tanzania kupata msaada wa madume 11 ya ngombe bora wa kisasa ambayo yataongeza uzalishaji kutoka ndama laki moja hadi kufikia milioni moja kwa mwaka.
Akizungumza wakati anapokea madumehayo katika kituo cha taifa cha uzalishaji wa mbegu bora za mifugo(NAIC) kilichoko Usariver Mkoani Arusha waziri wa mifugo na uvuvi Mh Luhaga Mpina amesema hatua hiyo inayolengakuharakisha kuleta mapinduzi katika sekta ya mifugo.
Aidha Waziri mpina alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na kujenga misingi ya kuongeza thamani ya mazao yamifugo kwa wafugaji na pia Taifa kwa ujumla
Waziri Mpina alisema katika kuhakikisha hatua hiyo inatekelezwa tayariwizara yake imeanza mchakato wa kufanya utafiti wa kubainikama Tanzania yenye ngombe zaidi ya milioni 28 ina ulazima wa kuendeleakuagiza maziwa kutoka nchi za nje ama la.
"Tunataka kujiridhisha kuwa hivi ni kweli tunahitaji kuendelea kuagiza maziwa kutoka nje ?na hivi ni kweli kuwa sisi kama Taifa na wafugaji wetukwa ujumla kuna tija yauagizaji huo wa maziwa ama ni miradi ya baadhi yawatu ?" alihoji Mh Mpina
Katibu mkuu wa wizara ya mifugo Dr. Marry Mashingo amesema Madumehayo ambayo ni msaada kutoka mfuko wa Billgate yenye thamani yamilioni 242 yatasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwakwa wafugaji wenyewe na pia kwa wasindikaji
"Madume yotekumi na moja itaongeza dozi za mbegu zinazozalishwa kwakuweza kupata ngombe milioni13 katika kipindi cha miezi sita,hali hii itaharakisha kuongeza aina yangombe bora kwa wafugaji wetu"alisema Katibu Mkuu Dr. Marry Mashingo
Mkurugenzi mkuu wa utafiti wa mifugo nchini Dr Eligi MussaShirima amesema wamebuni mbinu mpya ya kuwafikishia wafugaji mbegubora kwa gharama ndogo ikiwemo yakutumia chupa maalumu zinazofanana na chupaza Chai hatua itakayorahisisha na kuwawezesha kupata mbegu hizo kwa wingina kwa wakati.
Baadhi ya wadau wa mifugo kutoka sekta binafsi wanasemahatua hiyo ya serikali imewapa matumaini makubwa na kwamba ikiweza kutekelezwakwavitendo itaharakisha mapinduzi yanayotarajiwa katika sekta ya ufugaji.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.