Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha kiasi cha shilingi Milioni 520 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chekeleni Wilayani Arumeru baada ya kukagua mradi wa Maji kwenye kisima cha mashine ya kusukuma cha Maji.
Amesema Serikali inaendelea kutatua changamoto ya Maji katika Mkoa wa Arusha na mradi huo mkubwa ukikamilika shida itakuwa imesha.
Nae, Waziri wa Maji Juma Aweso amesema Mkoa wa Arusha ulikuwa na changamoto kubwa ya Maji kwani upatikanaji wake ulikuwa ni 40% tu lakini kwa sasa Maji yanapatikana kwa 65%, hivyo ni juhudi kubwa za Serikali za kuhakikisha tatizo la Maji linaisha katika Mkoa wa Arusha.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema Chama kitahakikisha ahadi zote zilizowekwa kwenye ilani ya chama hicho zinatekelezwa na kukamilika ndani ya miaka 5.
Rais, Samia Suluhu Hassan ameanza ziara yake ya siku 2 katika Mkoa wa Arusha ambapo siku ya kwanza amekagua mradi wa Maji wa Chekeleni na kufungua Hospitali ya Jiji la Arusha iliyogharimu Bilioni 2.5 za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo na pia amekabidhi mfano wa hundi ya fedha za mikopo yenye thamani ya Bilioni 1.3 kwa vikundi vya kinamama, vijana na wenye ulemavu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.