Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewaagiza wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha utengenezaji wa madawati, Viti na Meza kwa ajili ya Madarasa uwende sambamba na ujenzi wa Madarasa hayo.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa Madarasa manne katika shule ya Sekondari Loliondo na ujenzi wa Madarasa mawili katika shule ya msingi shiniki Waso Wilayani Ngorongoro.
"Ninachotaka hapa ujenzi ukimalizika wa Madarasa, Viti, Meza na madawati yawe yamekamilika ili wanafunzi waingia kwenye Madarasa.
Haitakuwa na maana Madarasa yakamilike alafu tuanze zoezi la kutengeneza Viti, meza na madawati wakati vinaweza vikatengenezwa sasa kwani haviathili chochote katika ujenzi wa Madarasa.
Diwani wa kata ya Loliondo bwana Marekani Bayo amesema kata yake imepokea fedha Milioni 206 katika shule ya Sekondari Loliondo kwa ajili ya ujenzi wa bweni na Madarasa zaidi ya 6.
Bwana Bayo amesema zaidi ya Milioni 260 zimepokelewa katika kata yake kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule ya Loliondo, shule ya Julieth Kapunguni Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 2, zaidi ya Milioni 15 kwenye shule ya msingi Loliondo.
Ameishukuru Serikali kwa kuweza kuinua sekta ya elimu kwa kiwango kikubwa na kuwafanya wananchi wake watulie eneo moja badala ya kuhama hana kila mara.
.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.