Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka waoneshaji na wananchi kutumia fursa zilizopo kwenye kilimo ,uvuvi na ufugaji ile ziweze kuleta tija kwani fursa zinafuatwa na hazimfuati mtu.
Amewataka wataalamu wa sekta hizo husika wakajipange kutoa elimu katika maeneo yao badala yakusubiri maonesho ya nanenane ili wakulima na wafugaji wapate elimu hiyo.
Amesisitiza kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi amewashauri wananchi watumie fursa ya kilimo cha umwagiliaji zaidi kwani maeneo yapo yakutosha katika Mikoa yote mitatu.
Serikali ya Dkt. Samia imeendelea kutenga fedha zaidi katika sekta ya kilimo na kwa kanda ya Kaskazini zaidi ya bilioni 47.6 zimetolewa ili kukuza Kilimo zaidi hasa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.
Mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imepanga kuchimba visima takribani 150 kwa kila halmshauri ili kurahisha upatikanaji wa maji yatayorahisisha kilimo cha umwagiliaji.
Amezitaka Halmshauri zote kanda ya Kaskazini kutoa ushirikiano kwa tume ya uwagiliaji itakapoanza zoezi la kubainisha maeneo ya uchimbaji visima hivyo kwa kuwashirikisha wananchi.
Amewataka wafugaji kushirikiana na serikali katika kutumia teknolojia ya ufugaji wenye tija kwa kuwa na mifugo michache zaidi kutokana na upungufu wa maeneo ya malisho.
Kutunza mifugo michache ni rahisi zaidi kuliko mifugo mingi kwani gharama inakuwa chini na pia mfugaji atapunguza msongo wa mawazo.
Amewataka wakulima na wananchi kuona namna yakuongeza mnyororo wa thamani ili mazao yaweze kuleta tija zaidi.
Amezitaka Halmashuri kutunza fedha zinazotolewa kama ushuri unaotoka kwenye kilimo na uvuvi zirudi kwenye maeneo husika ili zikaleta mabadiliko zaidi kwenye maeneo hayo.
Akizungumza katika maonesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema maonesho hayo yataendelea kuboreshwa kila mwaka ili yaongeze tija zaidi kwa waoneshaji na wananchi.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Moshi Kisare Makori kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema maonesha haya yanawapa fursa wakulima na wafugaji wakuonesha mazao yao na pia kutoa elimu kwa wananchi.
Ameshauri SIDO kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara ili kuwapa elimu ya utengenezaji bora wa bidhaa itakayowawezesha kupata masoko yakutosha.
Pia, amewashauri Shirika la viwango Tanzania TBC kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara hao ili waweze kupata vibari vya ubora kwa haraka.
Hata hivyo, amezitaka halmshauri kupitia kwa maafisa ugani kutoka nje ya ofisi zao ili kutoa elimu yakutosha kwa wakulima kwa lengo la kuzalisha mazao yenye ubora na yatayokubalika katika masoko mbalimbali.
Nae, Mwenyekiti kamati ya maandalizi ambae pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amesema kwa maonesho ya mwaka 2023 jumla ya washiriki 220 kutoka Taasisi na Kampuni zimeshiriki katika maonesho hayo.
Maadhimisho ya siku ya wakulima na sherehe za nanenane Kanda ya Kaskazini yamefanyika katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha na yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo "Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula" na Mikoa iliyoshirikia ni Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.