Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Dkt.Seleman Jaffo amewataka wananchi wa wilaya ya Arumeru kuendelea kutunza vyanzo vya Maji kwa kupanda miti inayotunza Maji.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua vyanzo vya Maji ambayo yanatumika kwa kiasi kikubwa na Mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Arumeru.
Mabadiliko ya tabia nchi yanatulazimisha kuongeza nguvu zaidi ya kutuza vyanzo vya Maji ili vyanzo hivi viendelee kutumika hata baada ya miaka 50.
Aidha, amefurahishwa na namna Wilaya hiyo inavyoendelea kutunza vyanzo vya Maji kwani kuna maeneo mengine vyanzo vya Maji vimeshavamiwa na shughuli za kibinadamu lakini kwa Wilaya hiyo hali ni tofauti na vyanzo vya Maji vipo vizuri.
Waziri Jaffo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imeweka nguvu kubwa katika kutunza mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kivulinda zaidi vyanzo hivyo.
Hata hivyo, ameitaka halmashuri ya Meru kuongeza bajeti ya utunzaji mazingira kwani iliyopo sasa haitoshi kuhakikisha shughuli zote zinafanyika ipasavyo.
Nae,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng. Richard Luyago amemuwakikishia Waziri Jaffo kuendelea kutunza mazingira katika Wilaya hiyo na kuvilida vyanzo vya Maji.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.