Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dk.Athuman Kihamia amesema atashirikiana na Viongozi wote wa Mkoa wa Arusha ,wadau wa maendeleo na wananchi kwamba Umoja na mshikamano ndiyo silaha pekee ya maendeleo .
Dk.Kihamia akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Viongozi wa Serikali na wadau wa maendeleo waliojitokeza kumpokea alisema kuwa atafanya kazi na kila mtu katika Mkoa wa Arusha .
Alisema kuwa ni kweli katika Mkoa wa Arusha ni mwenyeji na kwamba sababu hiyo inampa fursa ya kufanya kazi na kila mtu na kudai kuwa nia ya Serikali nikuwaletea wananchi maendeleo kwamba tofauti zisizo na tija ziwekwe pembeni kazi ya maendeleo indelee .
Awali Mkuu wa Wilaya Arusha Kenan Kehongosi akimkaribisha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa John Mongela alimhakikishia ushirikiano na Umoja na kudai kuwa Viongozi wa Arusha wana Umoja na mshikamano
Mh.Kehongosi alisema kuwa maendeleo yeyote duniani yanategemea Umoja na mshikamano na kwamba Arusha umoja na mshikamano ni kipaumbele kwa kila mtu kwa sasa .
Katibu Tawala huyo alipokelewa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha , Dk.John Pima ,Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ,watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,na viongozi wengine ikiwa ni pamoja na kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha .
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.