Mkoa wa Arusha umeweka lengo la kupanda miti zaidi ya Milioni 10 kwa mwaka 2023, kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akishiriki siku ya upandaji Miti Kimkoa iliyofanyika katika halmashauri ya Arusha.
Mongella amesema swala la upandaji miti ni muhimu kwani miti inaleta uhai kwa binadamu kwa kutoa hewa safi.
Aidha, amewataka wakuu wa shule zote kwa kushirikiana na wadau wa misitu kuanza kampeni ya upandaji Miti katika maeneo ya Shule, Makanisa na Misikiti.
Amesema Miti ni chanzo cha Maji katika mazingira yetu hivyo inatakiwa kutuzwa na kulindwa.
Afisa Misitu Mkoa bwana Julias Achiula amesema changamoto kubwa inayopo katika sekta ya miti ni uvamizi wa maeneo ya misitu kutokana za shughuli za kibinadamu.
Pia, uwaribifu wa vyanzo vya Maji kwa ukataji holela wa miti.
Bwana Achiula amesema mpango uliopo katika ngazi ya Mkoa ni kuendelea kutoa elimu katika Jamii juu ya faida za upandaji miti na pia ufugaji wa kisasa ili kulinda misitu.
Siku ya upandaji Miti Kimkoa imefanyika katika halmashauri ya Arusha na jumla ya miti Milioni 1.8 imepandwa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.