Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewaasa wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa na moyo wa kusamehe ili kuachilia maumivu na kupata ahueni ya moyo.
Mhe. Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Arusha katika wiki ya haki inayotarajiwa kusitishwa leo ambapo amesema kuwa wakazi wa Arusha wanapaswa kuendelea kumuamini Mungu kwani yeye ni mtetezi wa wote.
Msisitizo wa Mhe. Makonda wa kuwaomba wananchi wa Mkoa huo kusamehe umekuja mara baada ya kugundua kuwa zipo kesi zinazohusiana na visasi ambazo sio nzuri kwa mustakabali wa jamii ya Mkoa huo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.