Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amewataka viongozi wa Mkoa Arusha wakiwemo wakuu wa Wilaya,wenyeviti wa Halmashauri na watendaji wote kusimamia miradi ya Maji ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa.
Maagizo hayo ameyatoa katika kikao kazi cha wadau wa maji wa Mkoa wa Arusha.
"Ili miradi hii iweze kukamilika inaitaji ushirikiano wa ngazi zote na wananchi watapata Maji kwa wakati".
Dhima ya Serikali ni kuhakikisha Maji mijini yanapatikana kwa asilimia 95 na Vijijini asimilia 85 ifikapo 2025, ndio maana fedha nyingi zimeletwa kwenye miradi hii.
Amesema wajibu wa viongozi ni kuhakikisha Maji yanawafikia wananchi kwa wingi.
Nae, Meneja anaesimamia vyombo vya watoa huduma za Maji ngazi ya jamii ambae amemwakilisha Meneja Mkuu wa RUWASA,bi Valentine Masanja amewaomba viongozi wa Mkoa wa Arusha kuwahamisisha wananchi wachangie bili za Maji ili miradi mingi iweze kuanzishwa na huduma za Maji kuwafikia wananchi.
Mhandisi Emmanuel Makaidi amesema maelekezo yote yaliyotolewa wanaenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Arusha wanapata Maji ya kutosha.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Frank Mwaisumbe kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wote amependekeza miradi mikubwa ya Maji ndio itatatua changamoto ya Maji kwa kiasi kikubwa hasa kwa Jamii za wafugaji kuliko miradi midogo inayowafikia wananchi wachache.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.