Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Felician Mtahengerwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na Kamati ya Usalama mkoa huo, mchana wa leo Agosti 12, 2024.
Dkt. Mpango yuko mkoani Arusha kwa ajili ya Kufungua Kongamano la Elimu ukanda wa Afrika Mashariki na Maadhimisho ya mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika kesho Agosti 13,2024, kwenye Kituo cha Mikutano Arusha (AICC)
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.