Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Felician Mtahengerwa na viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na Kamati ya Usalama mkoa huo, mchana wa leo 06 septemba, 2024.
Dkt. Mpango yuko mkoani Arusha kumuwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Jubilee ya miaka 50 ya huduma ya New Life Outreach Tanzania itakayofanyika 07 Septemba, 2024 katika ukumbi wa New Life Outreach , kwa Iddi Sakina Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.