Na Elinipa Lupembe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikagua mabanda kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi za Serikali kuhusu Utumishi wa Umma, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja na Wasimamizi wa Rasilimali Watu katika sekta za Umma Barani Afrika 2024, unaofanyika mkoani Arusha kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) mapema leo Novemba 04, 2024.
Mhe. Majaliwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Mkutano wa 9 unaofanyika kwa siku 4 kuanzia tarehe 04 - 07, Novemba, 2024.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Utawala Stahimilivu na Ubunifu; Kutunza Sekta ya Umma Ijayo Kupitia Uongozi wa Rasilimali Watu"
PICHA ZA MATUKIO
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.