*UGENI*
WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amewasili mkoani Arusha mchana wa leo na kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Kamati ya Usalama Mkoa, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kwenye Kiwanja cha Ndege cha Arusha, Aprili 11, 2024.
Mhe. Waziri Mkuu yuko Mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine itakayofanyika nyumbani kwake kijiji cha Enguik, kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli tarehe 12 Aprili, 2024
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.