.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Nafco, kata ya Olmot, halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, mwalimu msimamizi wa mradi huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mirongoine, Mwl. Edna Nasoro Makala, amesema kuwa, mradi huo unatelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 400 fedha kutoka Serikali Kuu.
Ameongeza kuwa, mradi huo utahusisha ujenzi wa jengo la ghorofa tatu, ambapo awamu ya kwanza utakamilisha ujenzi wa sakafu ya kwanza ukiwa na vyumba vinne vya madarasa na matundu 11 ya vyoo.
Hata hivyo, Diwani wa kata ya Olmot Mhe. Raphael Mathayo Lomwiko, licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule hiyo mpya, amesema kuwa watoto wa mtaa huo wanapata shida sana kutokana na eneo hilo kitokuwa na shule karibu ambapo hulazimika kutembea takribani Km 8 kufuata shule ya msingi Miroingoine.
"Kutokana na Jiografia ya kata hii, miaka ya nyuma eneo hili lilikuwa na mashamba yaliyomilikiwa na kampuni ya NFCO, hivyo hakukuwa na shule karibu, kwa sasa yameanza kuwa makazi ya watu, hivyo kuna uhitaji mkubwa wa shule kwa ajili ya watoto wa eneo hili" Ameweka wazi Mhe. Diwani.
Ameongeza kuwa, uwepo wa shule hapa utapunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule ya msingi Mirongoine lakini zaidi itapunguza utoro kwa wanafunzi wanaoshindwa kuhudhuria masomo kwa siku zote kutokana na umbali sambamba na mdondoko wa wanafunzi shuleni.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.