Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda @kea amewataka Wafanyabiashara waliofika kwenye hafla ya Koneksheni iliyowakutanisha na Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini Tanzania kutokumchukulia poa mtu yoyote aliyekaa nae karibu.
"Uliyekaa naye karibu yako, usimchukulie Poa anaweza akawa mtaji wako wa kesho, kwa kuwa hatima ya mwanadamu imeshikwa na Mungu" Amesisitiza Mhe. Makonda
Amewata wafanyabiashara hao, waliohudhuria hafla ya kula na kunywa pamoja kutumia fursa hiyo, kufahamiana, kubadilishana mawazo, uzoefu na kujadiliana masuala mbalimbali ya Biashara na Uwekezaji baina yao.
RC Makonda ameeleza mambo mengi ya msingi na ya kujifunza katika Hafla hiyo iliyofanyika Agosti 29, 2024 mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.