UTI NA KUTOKUSHIKA MIMBA, CHANGAMOTO KUBWA KWA WANAWAKE WA ARUSHA.
Epfania Massawe ni Afisa Muuguzi ambaye kazi yake kubwa kwenye Kambi hii ya Matibabu ya kibingwa Mkoani Arusha kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid imekuwa ni kutoa elimu kwa akinamama mbalimbali wanaofika hapa kwaajili ya kupata huduma mbalimbali za vipimo na matibabu ya kibingwa.
Afisa muuguzi huyo amesema changamoto kubwa waliyoibaini kwa akinamama wa Mkoani Arusha ni pamoja na matatizo ya mifumo ya mkojo (UTI), kutokushika ujauzito pamoja na upungufu wa damu kwa akinamama wengi wakati wa ujauzito.
Afisa huyo amewataka wanawake wa Mkoa wa Arusha kuwa na utamaduni wa kula mlo kamili hasa wakati wa ujauzito pamoja na kuhudhuria Kliniki pindi tu wanapobaini kuwa na ujauzito ili kuepukana na madhara na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuzuilika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.