Vijana nchini wametakiwa kutumia vizuri na kwa ungalifu mitandao ya kijamii, itumike hasa katika kujipatia elimu mbalimbali zakuwajenga na kuleta maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe alipotembele kituo cha redio cha Sunrise nakukutana na uongozi na wafanyakazi wa kituo hicho.
Amesema tayari sheria ya mtandao na kanuni zake ipo kwenye hatua za mwisho, hivyo amewataka watumiaji wa mitandao hiyo kuwa makini sana kwani sheria itakapoaanza haita mwacho yoyote ambae ataikiuka.
Nchi nyingi zinatumia hii sheria na Tanzania tulichelewa kuanza kuitumia,hivyo niwakati sasa wakuhakikisha maadili ya nchi yanazingatiwa na kufuatwa.
Pia amevitaka vyombo vya habari kufanya kazi kwa kufuata sheria na maadili ya nchi, ili kujenga vizazi vyenye kufanya kazi kwa weredi na heshima.
Aidha,amesema serikali inafanya kazi na vyombo vya habari kwa kufuata sheria ya uhuru wa habari, hivyo penye kutoa taarifa zinazowahusu wananchi itafanya hivyo ili wananchi waweze kufahamu kwa kina mambo yote yanayoendelea katika serikali yao.
Serikali ipo tayari kupokea taarifa yoyote inayokosoa kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo na kuweza kuifanyia kazi, ili kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Hata hivyo amesema, serikali haitafumbia macho chombo chochote cha habari kitakacho toa taarifa za uwongo na uchochezi,hivyo sheria itachukua mkondo wake.
Amesisitiza zaidi kwa wananchi wa Arusha kujifunza jinsi yakuboresha ujasiliamali ili uwe wakuwanufaisha hususani fursa za utalii na nyingine nyingi.
Dokta Mwakyembe yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3 ambapo atafungua mkutano wa Maafisa Habari nchini,atatembelea na kukagua uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid na atazungumza na wadau wa utamaduni,sanaa na michezo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.