Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi pindi itakapofika muda wakutoa maoni ya dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050.
Kauli hiyo ameitoa wakatika akifungua kikao maalumu cha uelimishaji wa uwandaaji wa dira ya Taifa ya maendeleo kwa mwaka 2050.
Amesema dira kazi yake kubwa nikuonesha wapi unakwenda na utakwendaje na unatarajia kufika lini.
"Kukosa dira nisawasawa na mtu ambae hajui anaelekea wapi na mtu kama huyu huwa hawezi kupotea maana anakuwa hajui wapi anaenda atakapochoka ndio atakuwa amefika".
Jukumu letu sisi viongozi kwanza, nikujenga uwelewa wa dira hii ya 2050 na kisha tutoke kwenda kwa wananchi na wale wote tunaowaongoza chini yetu kuwaelimisha na kuwahamasisha.
Mongella amesema, dira ya sasa inaelekea ukingoni ifikapo 2025 na mabadiliko makubwa tumeyaona katika nchi yetu kupitia sekta mbalimbali kama uchumi, afya, maji, umeme, elimu na miundombinu ikiboreshwa kila leo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa timu ya uandishi wa dira ya Taifa ya maendeleo 2050 Gladness Salema amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na akaona nivizuri asikilize wananchi wake wanataka nchi ielekee wapi kupitia mpango huu wa dira ya Taifa ya maendeleo 2050.
Vilevile, amewataka viongozi wa kisiasa washiriki kikamilifu katika zoezi hili la kihamasisha wananchi wachangie maoni ya dira ya Taifa 2050 ili waseme wanataka Tanzania ya namna gani.
Gladness amesema zama za manung'uniko na malalamiko zimepitwa ni wakati sasa wa kila mtu kusema anataka Tanzania ya namna gani.
Nae, Mjumbe wa timu uandishi wa dira ya Taifa ya maendeleo 2050 Sostenes Kewe amesema dira hii itaenda kutuunganisha wananchi wote kwani tutaweza kusema tunataka Tanzania ya namna gani.
Amesema, dira hii niyamiaka 25 hivyo itajikita kuonesha mabadiliko ya mazingira, vipaombele vya muda refu, itaweza kuonesha mwelekeo wa nchi, itaendeleza mafanikio ya dira 2025.
Kikao kazi cha dira ya Taifa ya maendeleo 2050 kimefanyika katika ngazi ya Mkoa wa Arusha na kujuisha viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na viongozi wa dini kwa lengo la kujengewa uelewa wa dhana nzima ya dira na namna watakavyoshiriki katika kujenga uwelewa kwa wananchi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.