Na Elinipa Lupembe
Viongozi wa mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, wameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. samia Suluhu Hassan, kwa kuupa hadhi mkoa huo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kimataifa, kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.
Wakizungumza wakati wa makabidhiano ya Hati Miliki ya eneo litakalojengwa uwanja hua, kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Damas Damian Ndumbaro (MB), alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi, viongozi hao, licha ya kuishukuru Serikali kwa maamuzi ya kuifanya Arusha, kuwa mwenyeji wa mashindao ya AFCON, wameweka wazi kuwa, mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa iliyonufaika sana na fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo Kisekta, ikiwemo miradi ya maji, afya, elimu, miundombinu ya barabara na umeme na sekta ya Utalii.
"Kwa niaba ya viongozi wa dini, chama na Serikali, Baraza la Madiwani Jiji la Arusha, Mhe. Mbunge Mrisho Gambo, pamoja na wananchi wote wa mkoa wa Arusha, tunaishukuru Serikali kwa kuamua na kuchagua mkoa wa Arusha kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCOM, tunaamini mashindano hayo yatakuwa chachu kwa maendeleo ya mkoa na chanzo kikubwa cha mapato, yatayokuza pato na uchumi wa mkoa pamoja na kuchochea ari katika sekta ya Utalii wa michezo pia ". Amesema Mhe. Mongella.
Aidha ameahidi kuilinda heshima waliyopewa na Mhe Rais, wao kama wanaArusha wamebeba dhamana hiyo, kuhakikisha uwanja unajengwa, licha ya kuwa tayari Eka 39 zimeshapatikana, Eka nyingine 44 zitapatikana kabla ya mwezi Machi 2024, taratibu zote zikiwa zimekamilika tayari kwa kujenga viwanja vinne kwa ajili ya mazoezi na kiwanja kimoja cha waamuzi wa mipra 'refferies' na kuwa na jumla ya viwanja vitano vyenye hadhi ya kimataifa.
Naye Diwani wa Kata ya Olmoth, Mhe. Raphael Mathayo Lukumay, amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia kwa kuipa kipaumbele Kata ya hiyo, kujengwa uwanja katani hapo na kuahidi kutoa ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa mrafi huo na pindi eneo litakapohitajika wananchi wapo tayari kupisha ili malengo ya serikali yao yaweze kutimia
"Tufikishie salama zetu kwa mama Samia, sisi wananchi wa Olmoth, tunamshukuru, tunampongeza kwa maamuzi ya kutujali wananchi wa Olmoth, angeweza kuamua kujenga maeneo mengine lakini amechagua Olmoth, amechagua Arusha, tunamuombea kila la kheri kwa mEnyenzi Mungu, tunamuunganmkono kwa kutekeleza Ilani ya Chama kwa kishindo, tutatoa ushirikiano wakati wote wa ujenzi hata shughuli za michezo ya kimataifa zitakapoanza". Amebainisha Mwenyekiti wa CCM kata ya Olmoth.
Mwenyekiti wa mtaa wa Murongoine, Mhe. Lucas Sabaya Lukumay, amewapongeza viongozi wote wa Serikali Mhe. Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Mongella, Mkurugenzi wa Jiji na madiwani kwa umoja wao, wa kuwaongoza vema na kuhakikisha mradi huo unafanyika kama yalivyo maelekezo na kuongeza kuwa wananchi wa mtaa na kata nzima wako tayari kupokea mradi huo mkubwa na wa kimataifa.
#ArushafursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.