Na Elinipa Lupembe
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Dkt. John Danielson Pallangyo, amesema kuwa viongozi wa wananchi wanalojukumu la kuzingatia matumizi ya Takwimu sahihi za Matokeo ya Sensa ya Watu na makazi ili kupanga shughuli na kufikia malengo ya Serikali.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa makundi mbalimbali ya kijamii mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa AIM MALL Jijini Arusha leo tarehe 11 Desemba, 2023, Dkt. pallangyo amewataka viongozi walioshiriki mafunzo hayo kuyazingatia ili kwenda kuelimisha jamii namna na faida ya matumizi ya Takwimu hizo.
Ameweka wazi kuwa, Takwimu za Matokeo ya Sensa licha ya kuwa ni Dira ya maendeleo ya Taifa, lakini viongozi na watanzania wanalojukumu ya kuzitumia ili ziweze kufikia malengo ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Serikali.
"Kwa niaba ya wananchi wa Arumeru Mashariki, tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita, kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kisekta katika jimbo langu, ipo miradi yenye kutumia fedha nyingi a,bayo imetekelezwa na kukamilika huku ikitoa fura kwa wananchi kuitumia na kupata huduma ndani ya maeneo yao, ile hali ya wananchi kuuza vitu na mali zao ili kujenga madarasa kwa sasa kwetu imekuwa ni histori, Serikali imejenga madarasa mengi, tunamshukuru Mhe. Rais Samia, na niwatake wanaArumeru wote kumuunga mkono" Amebainisha Mhe. Dkt. Pallangyo
Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Rasilimali Watu, mkoa wa Arusha, David Lyamongi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, ukiwa na lengo la kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii juu ya matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022.
Makundi hayo ni pamoja na viongozi wawakilishi wa wananchi, viongozi wa Siasa, dini na mila, Watendaji wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata, kamati ya Sensa Mkoa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo watu wenye mahuitaji maalum.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.