Halmashauri YA Wilaya Ngorongoro
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Murtallah S. Mbillu amefungua na kushiriki kutoa mafunzo katika semina ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Waandikishaji na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni, pamoja na miongozo.
Aidha, Bw. Sadiki ametoa mafunzo hayo leo Oktoba 6, 2024 na amesema kuwa Waandikishaji wote wanapaswa kuwa waadilifu bila kumuonea mwananchi yoyote mwenye sifa za kuandikishwa.
"Katekelezeni majukumu yenu kama miongozo inavyowataka, sheria, kanuni na kwa kuzingatia kiapo mlichokula leo, pia kaonyesheni uaminifu mkubwa kama mlivyoaminiwa na kuchaguliwa kuwa waandikishaji".
Ikumbukwe zoezi la uandikishaji Wapiga kura litaanza tarehe 11 hadi 20 oktoba na Uchaguzi wa kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 27 Novemba, 2024 kwenye Tarafa zote tatu ambazo ni Loliondo, Sale na Ngorongoro.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.