Sekta ya elimu Mkoani Arusha inaendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na taasisi nyigi za elimu kutoka ngazi zote.
Kauli hiyo imesema na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella alipokuwa akifungua kongamano la elimu la kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere.
Katik kumuenzi Mwalimu nyerere aliyeweka nguvu kubwa katika elimu Mkoa wa Arusha unaenda kufuta changamoto ya upungufu wa Madarasa kupitia Serikali ya awamu ya sita.
Amesema kwa mwaka 2022/2023 Mkoa umepokea kiasi cha Bilioni 5.369 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya sekondari 268.
Kwa upande wake, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daniel Ole Njoolay amesema jambo la kuendelea kumuenzi mwalimu kupitia elimu ni nzuri sana maana ametuachia tunu nzuri ya kutumia elimu kama nyenzo ya kujikomboa.
Nae, Professa Nuhu Hatibu kutoka Shule ya Arusha Sayansi amesema mfumo wetu wa elimu unatakiwa ujikite zaidi katika kutengeneza wabunifu na wavumbuzi zaidi kuliko watoa huduma ili waweze kwendana na dunia ya sasa.
Afisa Elimu Mkoa wa Arusha bwana Abel Ntupwa amesema ufaulu kwa Mkoa wa Arusha kwa sasa umefikia wastani wa 89-94 kwa madarasa yote ya Mitihani.
Amesema kwa upande wa elimu bila malipo kwa mwaka 2021 Mkoa uliandikisha wanafunzi takribani 57408 na mwaka 2022 wanafunzi 59476 waliandikishwa ikiwa kuna ongezeko la uwandikishaji.
Mkoa wa Arusha ili uendelee kufaulisha zaidi umejipanga kuondoa daraja la 4 kwa madarasa yote ya mitihani na kuboresha zaidi mazingira ya kufundishia na kufundishiwa.
Kongamano la elimu la kumuenzi Hayati mwalimu Nyerere limejumuisha wadau mbalimbali wa elimu kwa lengo la kujadili mipango mbalimbali ya kuboresha elimu Mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.