Wafanyabiashara wa soko la Kilombero, Jijini Arusha, wamemsimamisha Mkuu wa mkoa huo, Mhe. John V.K Mongella na kuwasilisha ombi lao la kuruhusiwa kufanya biashara maeneo yote kipindi hiki cha sikuu ya Krismass ili kuwafuata wateja.
Mhe. Mongella amewataka wafanya biahsara hao, kutii sheria kwa kufanya biashara kati maeneo rasmi yaliyotengwa na Serikali kwa kuwa wateja huwafuata mahali waliko.
Aidha amemuagiza mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa kukaa na wafanyabiashara hao, kusikiliza kero na changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua ili wafanye biashara zao kwa amani na utulivu.
Wafanya biashara hao, wamesimamisha msafara wa Mkuu wa mkoa huo, wakati akitokea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la OPD, kituo cha Afya Levolosi.
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.