Na. James K. Mwanamyoto
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa madereva wa bodaboda kupunguza ajali zinazoepukika.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo akiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na Bajaji wa jiji la Dar es Salaam.
“Tumesikia hapa takwimu za ajali na vifo vinazotokana na ajali za bodaboda nchini, hivyo Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wekeni utaratibu wa kutoa mafunzo ya usalama wa afya za maafisa usafirishaji hawa wa bodaboda ili waepukane na ajali,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo lake la mafunzo, ili yaanze kutolewa mapema iwezekanavyo kwa lengo la kuepusha ajali na kulinda uhai wa madereva bodaboda na wasafiri wanaotumia vyombo hivyo ambao wengi wao ni nguvu kazi ya taifa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.