Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewataka wananchi Mkoani Arusha kuunga mkono, juhudi za wawekezaji wanaowekeza kwenye Mkoa huo, ili kukuza pato la mtu mmoja mmjoja la mkoa na kukuzauchumi wa Taifa, unakwenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Mhe. Mongella amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mgahawa wa KFC tawi la Arusha, Hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Mgahawa huo eneo la Clock Tower, Jijiji Arusha.
Amesema kuwa, wakaz wa Arusha wanatakiwa kufahamu kuwa, uwekezaji wowote nchini ni nguzo kubwa ya kuinua uchumi na kuboresha ukuaji wa teknolojia, kwa kuwa wawekezaji wanapowekeza wanaibua Teknolojia Mpya, ambazo zinawawezesha vijana wengi kujikwamua kiuchumi.
“Niwapongeze sana KFC kwa kuanzisha huduma hii muhimu kwenye mkoa wetu, kwa kuzingatia pia huu ni Mkoa wa kitalii hivyo watalii na wananchi wengi watavutiwa kupata huduma ya uhakika na kutoa ajira kwa Watanzania, sisi kama Mkoa tunaahidi kuwapa ushirikiano Mkubwa katika jambo lolote mtakalohitaji”. Amesema mhe. Mongella.
Ameongeza kuwa, uwekezaji huo umetokana na uwepo wa mazingira mazuri yaliyoboreshwa kulitia Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu hassana kwani huduma hiyo itawezesha uchangiaji wa pato la taifa na Jamii kwa ujumla kwa kulipa kodi ya Serikali
Akimzungumzia uamuzi wa kufungua tawi la KFC Jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works,Vikram Desai amesema hiyo ni hatua muhimu kwa Tanzania kuwafikishia wananchi huduma bora ya chakula lakini pia inachagia ajira kwa watanzania.
"Kuwepo kwa KFC Arusha kutawapatia wananchi huduma bora za chakula chenye hadhi ya kimataifa kwani mgahawa huu upo zaidi ya nchi 140 hivyo watalii wakifika Arusha watakutana na mgahawa huo na kufurahi Zaidi." Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta amesema kampuni hivyo imejipanga kuhakikisha Tanzania inashirikiana na kampuni ya Dough Works Tanzania katika kuhakikisha huduna ya KFC inatolewa kwa ufanisi ambapo Meneja masoko wa KFC alitoa ombi kwa wakazi wa Arusha kutumia vyakula vya KFC vinavyouzwa kwenye migahawa huyo iliyopo nchini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.