Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh.John Mongella amekuwa mgeni rasmi katika sherehe maalumu iliyoandaliwa na madiwani wa Jiji la Arusha chini ya uongozi wa Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa jiji la Arusha.
Lengo la sherehe hiyo ni kutoa motisha kwa waalimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jiji la Arusha kwa kutoa zawadi kwa waalimu ambao masomo yao yamefanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.
Mh.John Mongella amewapongeza madiwani kwa kuandaa siku hiyo na pia amewapongeza waalimu kwa jitihada zao katika elimu.
Aidha, Mongella ameomba halmashauri nyingine za mkoa wa Arusha waige mfano kwa halmashauri ya jiji.
Waalimu wameishukuru sana ofisi ya mkoa na halmashauri ya jiji la Arusha kwa kuwaandalia siku hiyo lakini pia wamemshukuru Rais Mh.Samia Suluhu kwa kuwapandishia mishahara kwa asilimia 23.3 na kuongeza kiinua mgongo kutoka 15% mpaka 33%.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na akiwemo Mbunge wa Arusha mjini Mh.Mrisho Gambo,Meya wa jiji la Arusha, Mkurugenzi wa jiji waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata na wadau mbalimbali wa elimu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.