"Jumla ya wanafunzi 1,073,941 wameshaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Mwaka 2023".
Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema wanafunzi hao wote wanatakiwa kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza mapema Januari 9, 2023.
Amesema idadi hiyo imejumuisha wavulana 514,846 na wasichana 559,095 ikiwa ni ongezeko la ufaulu wa wanafunzi 166,139 sawa na 18.3% ambapo kwa mwaka 2022 waliojiunga na kidato cha kwanza walikuwa 907,802.
Miongoni mwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wapo wanafunzi wenye mahitaji maalumu 2,775 sawa na 0.26% ikijumuisha wavulana 1,491 na wasichana 1,284.
Mhe.Kairuki amewataka wanafunzi wote waliopangiwa shule za bweni 4,224 kulipoti shuleni ifikapo Januari 7,2023 na wale wa shule za kutwa 1,069,717 sawa na 99.61% kulipoti shule ifikapo Januari 9,2023.
Vilevile, ameagiza uwandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kukamilika ifikapo Disemba 31,2022.
Aidha, amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha miundombinu yote ya shule inakamilika ifikapo Disemba 24,2022 ili kuruhusi wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo yao mapema Januari 2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.