Zaidi ya wananchi 4,210 wa kijiji cha Kilima Moja kata ya Rotia wilaya ya Karatu, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwasaidi kukamilisha ujenzi wa zahanati na kuweza kupata huduma bora za afya karibu, ikiwemo huduma za kinamama na mtoto sanjari na kuwapunguzia umbali kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Wametoa shukrani hizo, wakati Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava, alipofika kijijini hapo, kwaajili kukagua na kuwekaji wa Jiwe la msingi katika zahanati hiyo.
Christina Jakebi mkazi wa kijiji cha Kilimamoja, amekiri kijiji hicho kwa na changamoto ya muda ya mrefu ya upatikanaji wa huduma za afya hali iliyowasababisha kufuata huduma za afya kwenye hospital ya Kanisa la Lutheran huku wajawazito wakijifungulia nyumbani na wengine njiani kutokana na umbali.
Christina ameshukuru uwepo wa zahanati hiyo, ambayo wanatarajia kupata huduma kwa ukaribu, hasa wakati wa usiku kwa wanawake wanaotaka kujifungua.
"Tunashukuru uwepo wa zahanati kijijini kwetu, tunaomba ujenzi umalizike mapema ili huduma za afya zianze kutolewa kituoni, sababu Rais Samia Hassan Suluhu amedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wa wananchi "
Naye Kiongozi wa mbio za mwenge uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava alisema zahanati hiyo itasaidia wananchi kupata huduma za afya na kuwaagiza wakamilishe mradi kwa wakati ili huduma za afya zianze kutolewa .
Amewasihi wananchi kujitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa n8 uchaguzi muhimu ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali wanachaguliwa na kuagiza wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo hususaniwanawake na vijana.
"Niwasihi wananchi mjitokeze kusikiliza Sera za kila Chama na hatimaye kuchagua viongozi bora ikiwemo mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria pamoja na kupambana na Rushwa na dawa za kulevya.
Akiwasilisha taarifa ya mradi, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kilima Moja, Samwel Paulo amesema ujenzi huo ulianza mwaka 2019 kwa nguvu za wananchi wakijichangisha shilingi milioni 19 na hatimaye Serikali Kuu kuongeza milioni 50 na kufikia jumla ya milioni 69 .44.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.