Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewataka washiriki wa riadha wanajiandaa vizuri ili kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika mashindano ya riadha (Ngorongoro Marathon).
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanariadha wa mbio za Ngorongoro Marathoni wilayani Karatu.
Amesema riadha ni mchezo unaotoa ajira kwa vijani na hivyo kuwafanya waache hali ya utegemezi na kukuza uchumi wao.
Nae, Kaimu Kamishina wa uhifadhi kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Ephraim Mwangomo, amesema lengo kubwa la kufadhiri mashindano hayo ni kuhamasisha utalii wa ndani.
Pia, kuongeza uhifadhi kwa kuzuia ujangili ili kukuza utalii kwa kuwatunza wanyama pori.
Aidha, kamishina Mwangomo amesema, mashindano hayo yameweza kuibua vipaji vingi vya vijana ambao wapo walioweza kushiriki mashindano ya Kitaifa na Mataifa.
Ngorongoro Marathoni ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2008 na mpaka sasa mashindano hayo yameshatimiza miaka 12.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.