"Wananchi wanasubiri kupatiwa huduma iliyobora hasa wakinamama na watoto, hivyo jitaidini kukamilisha majengo ya mama na Mtoto haraka ili yaanze kutoa huduma".
Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika halmshauri ya Arusha.
Miradi ya hospitali niyakukamilika mapema sana ili wananchi waanze kupata huduma za afya kwa karibu zaidi na kuwapunguzia hadha ya kutafuta huduma hiyo mbali zaidi.
Pia miradi hiyo ikikamilika kwa wakati itasaidia thamani ya pesa kuonekana na miradi kuwa bora.
Ziara ya Katibu Tawala Mkoa ilijumuisha ukaguzi wa miradi ya afya na TASAF katika halmshauri hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.