Watu kumi na tano wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyohusisha lori na magari mengine matatu katika eneo la by Pass Ngaramtoni, wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na akiwa eneo la ajali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamshna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea Majira ya saa 11 jioni, Februari 24,2024, ambapo Lori lenye namba za usajili KAS 943, likiwa na Tela lenye namba TF67, likitokea Namanga lilipoteza mwelekeo na kugonga magari na kusababisha vifo vya watu 15 na majeruhi kadhaa.
Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa Mount Meru, huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitamini hapo.
Kamanda Masejo amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wakina ajali hiyo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Aidha amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mount Meru kutambua miili ya waliofariki katika ajali hiyo.
Bwana Ametwaa Jina Lake lihimidiwe
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.