Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angela Kairuki ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuratibu kikao kazi (Retreat) kwa viongozi na watendaji wa Mkoa wa Arusha nakuwataka wakitoka katika kikao hicho wawe kitu kimoja.
Waziri Kairuki ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika Wilayani Karatu.
Amesema kikao hicho kitawasaidia kujifunza zaidi mifumo iliyopo katika Serikali ili wawezi kuisimamia vizuri na kuitumia kwa ufanisi zaidi.
Pia, amewataka viongozi na watendaji ngazi ya Wilaya na Halmashauri kuelezea miradi inayotekelezwa na Serikali kwa wananchi huku wakiwashirikisha ili waweze kuwa na ufahamu zaidi.
Mhe. Kairuki amewataka Wakuu wa Wilaya kuongeza kasi ya kusikiliza kero za wananchi hasa kwa kuanzisha kliniki zinazotembea mtaa kwa mtaa ili na kutatua kero hizo.
Vilevile, amezitaka halmashauri za Mkoa wa Arusha kubaini vyanzo mbalimbali vya mapato nakuviwekea mikakati yaukusanyaji kwa wakati wote.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema lengo kubwa la Kikao hicho ni kuwa na uwelewa wa pamoja na kujipanga kama timu kutekeleza malengo ya Mkoa.
Mongella amesema kikao hicho kitaleta mabadiliko makubwa kwa viongozi hao na watendaji katika utendaji wao wa kazi nakuleta ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amesema kikao hicho kitawasaidia viongozi na watendaji kutoendelea kufanyakazi kwa mazoea.
Akizungumzia mafanikio ya Wilaya ya Karatu Mkuu wa Wilaya hiyo Horace Kolimba amesema Serikali imeweza kukuza uchumi wa Wilaya hiyo kupitia utalii ambapo watalii waliopokelea ni takribani 142,000 na kuingiza pato bilioni 27.
Kikao kazi hicho kimejumuisha Viongozi wa Mkoa, Wilaya,Halmashauri na taasisi za Serikali na mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo matumizi ya teknolojia ya TEHEMA na tathimini ya utendaji kazi kwa mwaka 2022/2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.