Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasili wilayani Monduli na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shemu Kiswaga na viongozi wa Chama na Serikali mapema leo Septemba 19,2024.
Mhe. Mchengerwa yuko wilayani Monduli kwa ziara ya Kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua mradi ya maendeleo kisekta.
Mhe. Mchengerwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda atatembelea mradi wa upanuzi wa hospitali ya wilaya ya Monduli na kuzindua jengo la wagonjwa wa nje OPD pamoja na kuzungumza na wanachi kwenye Mkutano wa Hadhara utakaofanyika kata ya Mto wa Mbu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.