Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), amewasili mkoni Arusha asubuhi ya leo, na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, kwenye uwanja wa Ndege Arusha, kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, amepokelewa mkoani Arusha, akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Manyara, eneo la Kateshi na Gendag wilaya ya Hanang, kutembelea na kuwajulia hali waathirika wa Maafa yaliyotokana na mvua kubwa, zilizonyesha usiku wa kuamkia tarehe 03 Desemba, 2023
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.