Na Elinipa Lupembe
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), amewasili mkoni Arusha na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella pamoja na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (MB) kwenye uwanja wa Ndege Arusha, kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania, asubuhi ya leo 22.11. 2023.
Akiwa mkoni Arusha, Mheshimiwa Waziri Mkuu atafungua, Maonesho ya 3, ya Wiki ya Huduma za Kifedha mwaka 2023, yanayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini Arusha.
Aidha, katika Mapokezi hayo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, ameambatana na Kamati ya Usalama mkoa, Viongozi wa chama na Serikali wa mkoa huo wa Arusha.
Awali, maonesho hayo yakiwa na lengo la kutoa Elimu kwa Umma, juu ya Huduma za kifedha pamoja na kuwajengea uwezo wa kuelewa, matumizi sahihi ya huduma rasmi za kifedha, zitakazosaidia katika utunzaji wa fedha zao, matumizi ye fedha, kuweka na kukopa, ili kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Kifedha Mwaka 2023 ni “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.